JOE COLE KUTIMKIA WEST HAM, BA KARIBU CHELSEA

BA

Kiungo wa Liverpool aliyecheza Lille kwa mkopo msimu uliopita Joe Cole anatrajiwa kuihama Liverpool na kujiunga na klabu yake ya zamani West Ham. Taarifa zilizotoka katika vyanzo mbalimbali vinadai kuwa kiungo huyo aliyekosa nafasi ya kudumu Liverpool yuko katika vipimo vya afya yake kabla ya kusaini kuichezea West Ham. Kwa upande nwingine mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal Papiss Demba Ba anahusishwa na mpango wa kuhamia Chelsea baada ya mazungumzo baina ya pande hizo mbili kuanza upya. Mazungumzo ya  Ba kwenda Chelsea yalivunjika kabla ya kuanza tena. Taarifa za mwisho zilisema kuwa Demba Ba atafanya vipimo leo na kumalizia taratibu zingine kabla ya kuhamia rasmi Chelsea. Uhamisho huo unatarajiwa kuigharimu Chelsea  kiasi cha pauni milioni 7
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates