WILSHERE KUSAINI ARSENAL


Baada ya kuwa katika mfululizo wa matokeo mabovu pamoja na tatizo la wachezaji nyota kuhama katika misimu ya hivi karibuni Jack Wilshere amesema ya moyoni na kusema nia yake ya kubaki Arsenal. Wilshere aliwasili Arsenal akiwa na miaka 9 na anataka kubaki Arsenal licha ya klabu hiyo kuonekana kupoteza mwelekeo. Jack ameongeza kuwa anataka kutimiza ndoto ya kuwa nahodha wa Arsenal, mkataba wa Wilshere unaomlipa pauni 50,000 kwa wiki unatarajiwa kumalizika 2017 na anahitaji kusaini mkataba wa miaka 4 utakaomweka klabuni hapo hadi 2021.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates