Home Unlabelled STERLING KUSAINI TENA LIVER
STERLING KUSAINI TENA LIVER
By burudanibuzz At December 20, 2012 0
Kinda wa Liverpool Raheem Sterling anatarajiwa kusaini mkataba mwingine utakaoendelea kumweka Anfield. Kinda huyo mzaliwa wa Jamaica alisajiliwa Liverpool mwaka 2010 akiwa na miaka 16 tu akitokea QPR na amepata nafasi nyingi msimu huu. Raheem ambae pia ni winga wa timu ya taifa ya England chini ya miaka 21 analipwa mshahara wa pauni 2000 kwa wiki ambao unakadiriwa kuwa milioni 3 za ki-Tanzania na ili kusaini mkataba mwingine anahitaji pauni elfu 50 kwa wiki. Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers amesema hakuna tatizo katika majadiliano ya mkataba na Sterling anaweza kusaini ndani ya masaa 24 yajayo.