Home Unlabelled SCHOLES AFIKIRIA KUSTAAFU TENA
SCHOLES AFIKIRIA KUSTAAFU TENA
By burudanibuzz At December 20, 2012 0
Kiungo mkongwe wa Manchester United Paul Scholes anapanga kustaafu tena soka na kuendelea na shughuli zingine za soka. Scholes alitangaza kustaafu kwa mara ya kwanza May 31 2011 kabla ya kurejea uwanjani kuokoa jahazi Januari mwaka huu. Scholes mwenye miaka 38, amecheza Man United katika kipindi chote cha maisha yake ya soka huku akitajwa kuwa miongoni mwa viungo bora kabisa katika kipindi chake cha uchezaji.Paul Scholes amefanikiwa kupata vikombe 10 vya ligi kuu, 2 vya UEFA pamoja na vikombe vitatu vya FA.