Home Unlabelled MAN U PABAYA 16 BORA
MAN U PABAYA 16 BORA
By burudanibuzz At December 20, 2012 0
Droo ya kupanga timu zitakazochuana kuingia nane bora imefanyika ambapo klabu ya Manchester united itakua na kibarua kizito mbele ya Real Madrid. Mechi ya Man U na Real imevuta hisia za watu wengi huku Barcelona na AC Milan ikiwa ni mechi nyingine inayotabiriwa kuwa ngumu na ya kusisimua. Christiano Ronaldo atacheza dhidi ya timu yake ya zamani huku mahasimu Jose Mourinho na Alex Ferguson wakikukmbushia enzi za uhasama wao Mourinho alipokuwa anainoa Chelsea. Barcelona itakua na kibarua kwa Milan ambayo ilikutana nayo kwenye mwezi wa pili msimu uliopita wa UEFA ambapo Barcelona ililalamikiwa kupita kwa msaada wa refa.Arsenal nayo ina shughuli pevu mbele ya Bayern Munchen ambao kwa njia yoyote watakua na machungu ya kukosa kombe hilo kwenye ardhi ya nyumbani kwao mbele ya Chelsea mapema mwezi wa 5 mwaka huu.