Lionel Andres Messi mchezaji anayesemekana kuwa bora ulimwenguni kwa sasa amesaini mkataba mpya utakaombakiza Camp Nou hadi mwaka 2018. Messi ambae hivi karibuni alivunja rekodi ya gwiji wa Ujerumani Gerd Mueller ya kufunga magoli mengi ndani ya mwaka mmoja amesaini mkataba huo huku wachezaji wengine maarufu wa Barca Carles Puyol na Xavi Hernandez pia wamesaini. Mkataba wa Xavi na Puyol utamalizika mwaka 2016. Messi anawania kupata tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa mara ya 4 mfululizo huku akiwa na kazi ya kumpiku Christiano Ronaldo na mchezaji mwenzake wa Barca Andres Iniesta waliobaki tatu bora.