Home Unlabelled MAN CITY CHALI
MAN CITY CHALI
By burudanibuzz At December 09, 2012 0
Klabu ya Manchester City jana imepata kichapo cha 3-2 kutoka kwa watani wao wa jadi Manchester United katika pambano lilochezwa Etihad. Manchester United walianza kufunga magoli mawili yaliyofungwa na Wayne Rooney dakika ya 16 na 29 kabla ya Yaya Toure kurejesha goli moja dakika ya 60. City walisawazisha kupitia kwa beki Pablo Zabaleta dakika ya 86 kabla ya Robin Van Persie kuondoa matumaini ya City kupata walau pointi moja alipopachika bao la tatu dakika 2 baada ya dakika 90 kumalizika. Baada ya mechi kwisha beki wa United Rio Ferdinand alipata majeraha ktk jicho lake la kushoto baada ya kurushiwa sarafu na mashabiki wa City.Kwa ushindi huo Manchester United imeendelea kushika usukani wa Ligi ikiwa na pointi 39, ikifuatiwa na City yenye pointi 33. Katika mechi nyingine iliyochezwa jana majogoo Liverpool walipata ushindi km wa United dhidi ya West Ham huku Tottenham ikichapwa 2-1 na Everton.