Baada ya kuzushiwa kifo mara kadhaa msanii Justin Bieber imegundulika yuko katika hatari ya kuuawa. Msanii huyo mwenye miaka 18 tu amejizolea umaarufu mkubwa hasa kutokana na shughuli za kimuziki, filamu pamoja na uhusiano wake na kinda mwingine supa staa Selena Gomez. Dana Martin ndiye anaesemekana kupanga suala hilo, aliyepewa jukumu hilo ni Mark Staake. Dana na Staake wote walikua gerezani kabla ya Staake kuachiwa huru.Taarifa za njama hizo zilitolewa na mpangaji wa njama hizo Dana Martin jambo lililosababishwa kushikiliwa kwa Staake siku ya tukio.
Home Unlabelled BIEBER HATARINI