KILIMANJARO STARS, HEROES WATOLEWA CHALENJI

Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes wametolewa katika michuano ya Tusker Senior Challenge Cup.  Kombe la Chalenji linafanyika nchini Uganda, Kilimanjaro Stars imetolewa na wenyeji Uganda baada ya kuchapwa huku Zanzibar Heroes ikitolewa kwa mikwaju ya penalti na Kenya licha ya kuanza kufunga. Khamis Mcha na Agrrey Morris wliifungia Heroes dakika ya 21 na 76 huku Nadir Haroub "Cannavaro" akijifunga na Mike Baraza kuwasawazishia Kenya. Zaznibar Heroes ilitolewa kwa mikwaju ya penalti huku mabao mawili ya Robert Ssentongo na moja la mshambuaji anayekipiga Simba Emmanuel Okwi yakitosha kufuta ndoto za wenzao Kilimanjaro Stars kuingia fainali.Fainali ya Chalenji itachezwa Jumamosi kati ya timu ya Kenya "HARAMBEE STARS" na Uganda "THE CRANES"
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates