Home Unlabelled RDM ATIMULIWA CHELSEA
RDM ATIMULIWA CHELSEA
By burudanibuzz At November 21, 2012 0
Klabu ya Chelsea imeendelea na utaratibu wake wa kutokuwa wavumilivu baada ya kumtimua Roberto Di Matteo leo. Di Matteo amefukuzwa baada ya mfululizo wa matokeo mabovu yaliyoikumba Chelsea katika siku za hivi karibuni. Chelsea ilitandikwa 3-0 na Juventus hapo jana katika hatua ya makundi jambo lililoweka nafasi ya Chelsea kutetea ubingwa wake kuwa finyu. Habari kutoka Chelsea zinadai Meneja mpya atatangazwa baada ya muda mfupi huku kocha wa zamani wa Barcelona Guardiola akipewa nafasi kubwa ya kuchukua majukumu hayo.