HARRY REDKNAPP ATUA QPR



MARK HUGHES

REDKNAPP MAZOEZINI LEO

Baada ya uvumilivu wa wamiliki wa QPR kwisha na kumtimua kocha Mark Hughes, aliekuwa kocha wa Tottenham Harry Redknapp ameonekana kuwa mtu sahihi kuchukua nafasi hiyo. Hughes alitimuliwa kutokana na mfululizo wa matokeo mabovu licha ya kutumia pesa kibao katika usajili wa nyota wengi akiwemo aliekuwa kipa namba moja ulimwenguni Julio Cesar. Redknapp kocha aliyeipa Tottenham mafanikio makubwa na kuifanya moja ya timu zinazoogopwa Uingereza anatarajiwa kurudi kufundisha soka baada ya kutimuliwa Tottenham baada ya kumalizika kwa msimu uliopita. Redknapp ana kazi ya kuhakikisha QPR wanasofanya vizuri baada ya timu hiyo kutoshinda hata mechi moja mpaka sasa.

Katika hatua nyingine, refa Mark Clattenburg atarejea katika soka kama kamisaa (FOURTH OFFICIAL) katika mechi itakayochezwa baina ya Tottenham na West Ham hapo Jumapili baada ya kufutiwa tuhuma za ubaguzi wa rangi dhidi ya kiungo wa Chelsea Mikel Obi. Ikumbukwe baada ya tuhuma hizo Clattenburg aliondolewa ktk orodha ya Waamuzi wa Ligi kuu ya Uingereza na Chama cha waamuzi nchini humo. Proffessional GameMatch Officials Board (PGMOB)
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates