Baada ya miaka 7 tangu afariki tarehe 11 Novemba 2004, mwili wa aliyekuwa waziri mkuu wa Palestina Yasser Arafat unatarajiwa kufukuliwa ili kupata ukweli wa kilichosababisha kifo cha kiongozi huyo. Tangu Arafat alipofariki kumekua na tetesi nyingi kuhusu kisababishi cha kifo chake huku suala la sumu likidokezwa kama sababu kuu ya kifo chake.Waziri mkuu huyo wa zamani wa Palestina alifariki Paris - Ufaransa mwili wake unatarajiwa kufukuliwa siku ya Jumannekwa ajili ya uchunguzi zaidi.