Katika show hii wasanii wengi wa HIP HOP walitisha mbaya na kuwafunika wenzao wanaoimba, Mabeste, Mwana FA, Stamina, Nikki, Joh, Ney ni baadhi ya waliofanya poa!! Kwa upande wa wanaoimba shangwe hazikua high.
TID ambae alifanikiwa kupa show moja ya Dar ni msanii aliyefanya performance bora miongoni mwa wasanii wanoimba huku akiwa na back up ya mtu mzima Ngwair alionyesha wazi ukongwe wake kwenye game alipiga bonge la show.
LIVE PERFOMANCE: Suala la live perfomance lilionekana chanzo cha kuondoa ladha ya music na kuwakosesha baadhi ya artists shangwe zilizotegemewa. Rich Mavoko,Dayna na Barnaba ambao walifanya shows kali mikoa mingine walishindwa kurudia hicho kitu Dar. Hii inaonyesha wazi kua Tanzania tunahitaji muda ili tuingie rasmi ktk Live perfomance.
Wasanii hawana budi kujipanga kwa ajili ya showz zao kwan perfomance ya Dayna na Barnaba ilikua Disaster ukilinganisha na shows zao zingine xo haifahamiki tatizo ni confidence au kuna kingine cha ziada!!!!
RICK ROSS: Alifanya poa na kupata shangwe kibao hasa alipopanda on stage na I`ma Boss,mwisho wa siku alionyesha difference japo si kubwa kivile ila aliwafanya waliolipa mkwanja au walositisha usingizi kutujutia.. "Its my first time here I feel so much LOVE" -RICK ROSS @Leaders Club
FIESTA TEAM: Team nzima ya Fiesta ilifanya kazi nzuri kuandaa show ya Fiesta,pongezi kwao japo kuna changamoto chache hasa ktk performance LIVE hope next time wataendelea kujizatiti!!!
WALIOFUNIKAAAAA
RECHO |
TID a.k.a MNYAMA |
MWANA FA |
MABESTE |
NEY WA MITEGO |