EL CLASSICO HAKUNA MBABE

 Ile mechi yenye ushindani wa kipekee iliyovuta hisia za wapenda kabumbu wengi kati ya Barcelona na Real Madrid CF iliyochezwa katika uwanja wa Nou Camp ilimalizika kwa sare ya timu hizo kufungana 2-2. Ronalfo na Messi wote walifunga magoli mawili kila mmoja katika mchezo huo.

Baada ya mchezo kocha wa Real Madrid Jose Mourinho aliwaaongelea Messi na Ronaldo kwa kusema "It should be prohibited to say which is the best in the world, They are both from another planet.",matokeo hayo yanamaanisha Barcelona inaendelea kushika usukani katika ligi hiyo ikiwa imewazidi Real Madrid kwa tofauti ya point nane.

Messi akishangilia
Real Madrid iko katika nafasi ya tano baada ya kuanza msimu vibaya,iko nyuma ya vinara Barcelona,Atletico Madrid,Malaga, na Real Betis. Kocha wa Barcelona amesema Messi anamfanya Ronaldo kuwa bora kutokana na changamoto anazopata kutika kwa Muargentina huyo. Mechi zingine zilizochezwa leo LA LIGA:
Levante 1-0 Valencia

Mallorca 1-2 Granada

Athletic Bilbao 1-0 Osasuna






Atlético Madrid 2-1 Málaga

Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates