Tottenham Hotspurs wamesogea mpaka nafasi ya tano baada ya kushinda 2-0 mbele ya Aston Villa,Steven Caulker na Aaron Lennon walifunga mabao yaliyowapa Tottenham ushindi huo muhimu. Mshambuliaji wa Newcastle Pappiss Demba Ba anaongoza katika listi ya wafungaji akiwa na magoli 6 akifuatiwa na Robin Van Persie, Steven Fletcher, Michu na Luis Suarez ambao wana magoli matano kila mmoja.
Lennon akifunga bao dhidi ya Aston Villa |