Home Unlabelled RIHANNA & CHRIS GETTING BACK
RIHANNA & CHRIS GETTING BACK
By burudanibuzz At October 08, 2012 0
Rihanna Robin Fenty mwanamuziki mwenye asili ya Barbados anayefanya kazi zake nchini Marekani amehit headlines za tabloids kwa mara nyingine baada ya kuvuja taarifa kuwa uhusiano wake na Chris Brown umerudi level. Kwa mujibu wa mtandao wa Hollywoodlife.com,Rihanna ameamua kumsamehe Chris na kumpa nafasi nyingine japo watu wengi hawamsapoti. Bosi wa Rihanna ambae pia ni mmiliki wa recording label inayomsimamia mwanadada huyo JAY Z, hapendi uhusiano huo kwani haoni sababu ya Rihanna kurudisha majeshi kwa Chris baada ya tukio la mwaka 2009.
Hata hivyo,Rihanna ambae naye breki hazikabi ameamua kujaribu bahati yake kwa mara nyingine kwa Chris huku kila mmoja akionekana wazi kukolea kwa mwenzie. Christopher Maurice Brown alizaliwa 5/5/1989 ni mdogo kiumri kwa Rihanna aliyezaliwa February 20,1988 lakini wanajaribu kuthibitisha alichoimba Aaliyah "AGE AIN`T NOTHING BUT NUMBER"
Rihanna na Chris walitengana kwa sababu ya role ya media na watu wengine waliokuwa karibu na kurudiana kwao ndo kuthibitisha kuwa hakuna anayeweza kuzuia penzi na WAKOSANAO NDIO WAPATANAO!!!!!!!!