LULU KALENDA TENA


LULU

  Ile kesi ya kuhusika na mauaji ya nguli wa filamu za Kibongo Steven Kanumba inayomkabili supastaa Elizabeth Michael almaarufu LULU imepigwa tarehe mpaka NOVEMBA 5atakapopandishwa tena kizimbani kujibu kesi inayomkabili. Lulu anatuhumiwa kuhusika na kifo cha Steven Kanumba mapema Aprili mwaka huu.
  Kesi hiyo inyoendeshwa katika mahakama ya Kisutu imehairishwa kutokana na maelezo ya wakili wa serikali Bwana Kenneth Sekwao kuomba kuhairishwa kwa kesi hiyo kwa kuwa upelelezi haujakamilika. Kesi hiyo ipo chini ya Hakimu mkazi Stuarti Sanga.

Kesi ya Lulu imevuta hisia za watanzania wengi kutokana na kuhusisha wasanii wawili wenye majina makubwa ktk soko la Filamu Tanzania.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates