SHERWOOD ATUPIWA VIRAGO TOTTENHAM

Mabosi wa Tottenham Hotspurs wamekubaliana kusitisha mkataba wa kocha Tim Sherwood kutokana na kutoridhishwa na kiwango kilichooonyeshwa na timu hiyo tangu Sherwood achukue nafasi ya Andre-Villas Boas miezi mitano iliyopita. Tottenham walimfuta kazi AVB baada ya mfululizo wa matokeo na mabovu na kumuajiri Sherwood ambae haakuisaidia sana Totts licha ya kumfufua mshambuliaji Emmanuel Adebayor ambaye kipindi cha Boas hakuwa na nafasi kwenye kikosi hicho. Kutimuliwa kwa Sherwood kumekuja siku moja tu baada ya West Bromwich Albion kumfukuza kocha wake pia.
Mkataba wa kocha huyo ulibakiza miezi 13 na kocha wa Southampton Mauricio Pochettino anatajwa kuwemo kwenye rada za Tottenham kuchukua nafasi ya Tim.Makocha wengine wanaotajwa ni pamoja na David Moyes aliyetimuliwa Manchester United, aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Jurgen Klinsmann pamoja, Frank De Boer na Rafael Benitez. Hata hivyo Pochettini atatakiwa kuilipa Southampton kiasi cha Euro milioni 2 endapo atavunja mkataba wake na Southampton ili kuhamia Tottenham. Pochettino amebakiza miezi 12 kwenye mkataba wake na Southampton ambao una kipengele kinachomlazimu kocha huyo kuilipa timu kiasi hicho cha pesa endapo atavunja mkataba kabla ya muda.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates