PSG WAMNYAKUA DAVID LUIZ

Paris Saint-Germain iko katika harakati za mwisho kupata saini ya mchezaji wa kimataifa wa Brazil anayekipiga Chelsea ya Uingereza David Luiz. Kukamilika kwa uhamisho hu kutamfanya David Luiz kuwa beki ghali zaidi ulimwenguni huku Chelsea ikipata zaidi ya mara mbili ya kiasi walichotumia kumnunua kutoka Benfica. Chelsea na Benfica zilifikia makubaliano ya Luiz kwa kiasi cha Euro milioni 21.3 January 2011. Uhamisho wa beki mwingine wa Kibrazil Thiago Silva kwenda PSG ndio unaoshikilia rekodi ya dunia kwa sasa na usajili wa Luiz utawafanya mabeki hao wawili wanaokipiga kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya Brazil kuwa pamoja.
Luiz ambaye anajiandaa kushiriki kombe la dunia na timu yake ya taifa anatarajiwa kukamilisha usajili huo unaokadiriwa kuwa na thamani ya Euro milioni 50. Mchezaji huyo mwenye miaka 27 ameandika shukran zake kwa Chelsea katika ukurasa wake wa twitter huku ukurasa wa Chelsea ukithibitisha makubaliano kati ya PSG na klabu hiyo ya London.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates