Richest actor #ShahRukhKhan's first salary was Rs 50! http://t.co/T4aKbI1Scb pic.twitter.com/DHJviv6Gjv
— TOI Entertainment (@TOIEntertain) May 24, 2014
Home Unlabelled HARD WORK PAYS-----SHAH RUKH KHAN "GLOBAL STAR"- MWIGIZAJI WA INDIA ANAYEWAKIMBIZA WAMAREKANI KWA PESA
HARD WORK PAYS-----SHAH RUKH KHAN "GLOBAL STAR"- MWIGIZAJI WA INDIA ANAYEWAKIMBIZA WAMAREKANI KWA PESA
By Iam Owino At May 24, 2014 0
Marekani inaongoza kwa kutengeneza filamu nzuri na lina soko zaidi ulimwenguni huku waigizaji wengi wakiwa na maisha ya kifahari ambayo kimsingi yametokana na kazi zao za sanaa lakini maili kibao kutoka Hollywood yupo jamaa ambaye kuna waigizaji wengi hawamfikii japo yeye hayupo Marekani. "Kuch kuch Hota Hai" karibu kila mtu anaifahamu kama sio filamu basi wimbo, sauti ya Shah Rukh Khan ambaye kwa mwaka huu ametajwa kuwa muigizaji namba mbili tajiri zaidi miongoni mwa waigizaji duniani. Ana miaka 48, amecheza filamu zaidi ya 50, amevunja rekodi kadhaa kwenye ulimwengu wa filamu India maarufu kama Bollywood, akiwa na tuzo kibao kuliko muigizaji yeyote wa kipindi chake India na bado ana mkwanja mrefu ambao unatokana na kazi zake za sanaa, umiliki wa timu ya kriketi Kolkata Night Riders, matangazo na biashara mbalimbali ikiwemo kampuni anayomiliki yeye na mke wake Gaurri Khan inayoitwa Red Chillies maalum kwa kutengenezza filamu.Shah Rukh ana utajiri unaokadiriwa kufikia dola milioni 600 anashikilia nafasi ya pili nyuma ya Jerry Seinfeld mwenye utajiri wa $ milioni 820. Nyuma yake kuna mastaa kama Tom Cruise, Tyler Perry, Johnny Depp na wengineo wengi ambao hawakufua dafu kwa staa huyo kutoka India. Shah Rukh ametoka mbali kimaisha kufikia mafanikio aliyonayo kwa sasa.