Home Unlabelled GIGGS ASTAAFU SOKA RASMI
GIGGS ASTAAFU SOKA RASMI
By Iam Owino At May 20, 2014 0
Baada ya mechi zaidi ya 900 akichukua vikombe zaidi ya 20 na kufunga magoli 168, Ryan Giggs hatimaye ameachana na soka. Giggs aliyeitumikia Manchester United kipindi chote cha uchezaji wake ameteuliwa kuwa kocha msaidizi kufanya kazi pembeni ya Louis Van Gaal aliyetangazwa kupewa nafasi ya kuinoa United kwa mkataba wa miaka 3. Giggs alikaa kwenye benchi la United kama kocha-mchezaji kumalizia msimu wa ligi baada ya David Moyes kufutwa kazi zikiwa zimesalia takriban mechi nne ligi kumalizika.Mchezaji huyo amefunga katika misimu 24 ya ligi kuu Uingereza ambayo ni rekodi kwa sasa.