ZAIDI YA 74 WAUWAWA NIGERIA

Zaidi ya watu 74 wameripoiwa kufariki baada ya mashambulio mawili yaliyotokea Kaskazini-Mashariki mwa Nigeria. Katika shambulio la kwanza kwenye kanisa katika jimbo la Adamawa, watu wapatao 22 waliuwawa kanisani. Tukio la pili lililogharimu maisha ya watu zaidi ya 52 katika jimbo la Borno lilifanyika sokoni ambako kulikuwa na mamia ya watu wakifanya shughuli zao za kila siku. Taarifa zinasema kuwa wanamgambo zaidi ya 50 wa Boko Haram walitega mabomu katika sokoni tukio lililoondosha maisha ya watu hao zaidi ya 50 huku wengine wakipata majeraha. Kundi la Boko Haram limehusishwa na mashambulio yote mawili.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates