Mkurugenzi wa Apple Inc. Tim Cook ameeleza kupanda kwa mauzo ya bidhaa za Apple huku mauzo hayo yakipanda kwa asilimia Amerika
Kusini kwa 76%, Afrika 65%, Japan 40%, Ulaya 115% na China mauzo yakipanda kwa 20%. Wachambuzi wa masuala ya biashara wanadai kuwa kwa Marekani pekee mauzo ya Apple yanazidi kushuka. Bidhaa ya mwisho kutengenezwa na Apple, Iphone 5 inafanya vizuri sokoni japo inakumbwa na ushindani mkubwa kutoka kwa Samsung S4 na simu ghali kuliko zote kati ya Iphone hizo ni Iphone 5s inayouzwa kwa $860 ambazo ni zaidi ya shilingi 1,300,000/=