CHELSEA YAMREJESHA MATIC STAMFORD BRIDGE

Klabu ya soka ya Chelsea inayonolewa na Jose Mourinho imeripotiwa kuwepo katika hatua za mwisho kumrudisha Darajani kiungo Nemanja Matic kwa ada ya uhamisho yenye thamani ya Euro milioni 22. Kiungo wa kimataifa wa Serbia aliondoka Chelsea kama sehemu ya uhamisho ulioigharimu Chelsea Euro milioni 25 wa beki David Luiz kutua Stamford Bridge. Kipindi cha mwaka 2011 ambapo usajili wa Matic kwenda Benfica ulifanyika, kiungo huyo alikadiriwa kuwa na thamani ya Euro milioni tano tu.
Uhamisho wa Matic utaleta changamoto kubwa sehemu ya kiungo huku John Obi Mikel na viungo wengine wakihitajika kufanya vema zaidi.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates