Home Unlabelled MAN U YAUA UJERUMANI
MAN U YAUA UJERUMANI
By burudanibuzz At November 27, 2013 0
Baada ya matokeo mabovu ya hivi karibuni huku ikishikilia nafasi ya ya sita kwenye ligi kuu ya Uingereza, timu ya Manchester United jana ilifaninikiwa kuifunga Bayern Leverkusen 5-0 na kuipa timu hiyo yenye maskani yake Old Trafford nafasi ya kusonga mbele kwenye hatua ya kumi na sita (16) bora. Chini ya kocha David Moyes, Mashetani wekundu hao walipata goli la kwanza kupitia kwa Antonio Valencia dakika ya 22 ya mchezo. Emir Spahic alijifunga dakika nane baadaye kuwaweka Man U 2-0. Wengine walioifungua United ni John Evans, Chris Smalling na Luis Nani.
Katika mechi zingine, Real Madrid bila nyota Cristiano Ronaldo iliifunga Galatasaray 4-1, PSG ikashinda 2-1 dhidi ya Olympiacos.