Home Unlabelled TABIA NJEMA SILAHA YA CONRAD MURRAY
TABIA NJEMA SILAHA YA CONRAD MURRAY
By burudanibuzz At August 02, 2013 0
Dunia nzima ilimfahamu huku watu wengine ha wakimlaani baada ya kusemekana alisababisha kifo cha mfalme wa Pop Michael Jackson mnamo mwaka 2009. Conrad Murray ambaye alikuwa daktari binafsi wa Michael alifunguliwa mashitaka na ilipofika Novemba 11,2011 majaji waliamua kumhukumu Conrad kwenda gerezani kwa miaka Minne. Ripoti za hivi karibuni zinadai jamaa huyo ataachiwa huru Oktoba 28 mwaka huu baada ya kuonyesha tabia njema na ya kuridhisha huko gerezani. Mama wa Michael, Catherine ameonesha kutoridhishwa na uamuzi wa kumwachia Conrad “It is not right I will never be able to see my son again, while his mother can see him.” amesema Catherine.
Conrad alishutumiwa kwa kumpa dozi kubwa MJ ambayo iligharimu maisha ya staa huyo ambaye dunia nzima ilimuomboleza.
