Jose Mourinho ameanza vizuri kampeni za kujiandaa na msimu mpya wa ligi baada ya timu yake kushinda 2-0 mbele ya Inter Milan ya
Italia kwenye mashindano ya Guiness International Champions Cup nchini Marekani. Oscar na Eden Hazard waliipatia Chelsea mabao hayo muhimu na kuifanya timu hiyo ya London kusubiri kucheza mechi dhidi ya AC Milan katika hatua ya nusu fainali. Mechi kati ya Chelsea na AC Milan itachezwa tarehe 4 huku hapo kesho Real Madrid itakipiga na LA Galaxy. Fainali inatarajiwa kupigwa tarehe 7 mwezi huu.