DROGBA AWALOWANISHA ARSENAL

Didier Drogba ameendelea kuonesha umwamba wake dhidi ya Arsenal baada ya hapo jana kufunga magoli mawili yaliyoipa timu yake ya Galatasaray ushindi wa 2-1 dhidi ya Arsenal kwenye Emirates cup. Drogba alifunga dakika ya 78 na 87 baada ya Theo Walcott kuifungia Arsenal dakika 40 ya mchezo. Galatasaray imebeba kombe la Emirates mbele ya wenyeji wao Arsenal huku Arsene Wenger akiendelea kufukuzia usajili wa mchezaji Luis Suarez.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates