VILANOVA AIACHA BARCA



GUARDIOLA & TITO
Timu ya barcelona imepata apigo baada ya kuthibitika kuwa kocha Tito Vilanova hawezi kurejea kuifundisha timu hiyo. Vilanova mwenye miaka 44 amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya koo anahitaji matibabu makubwa zaidi kitu ambacho kwa mujibu wa Rais wa klabu hiyo Sandro Rossel amesema halitampa muda wa kutosha kuiongoza timu hiyo. Desemba mwaka jana Tito alifanyiwa upasuaji mwingine baada ya ule wa 2011 akiacha timu chini ya kocha msaidizi Jordi.
Tito Vilanova alishikilia nafasi ya ukocha baada ya kuondoka kwa Pep Guardiola. Vilanova kwa kipindi cha misimu mitano alikuwa msaidizi wa Guardiola kabla y akocha huyo kuamua kuachana na kuifundisha Barca msimu mmoja uliopita.
Barcelona itatangaza kocha mpya ndani ya siku chache wakati timu hiyo ikipigana kufanya vema msimu ujao.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates