REINA KWENDA NAPOLI KWA MKOPO




Kuna makipa ambao watu wengi wanashangaa kwa nini wanacheza timu kubwa. Victor Valdes wa Barcelona na Pepe Reina ni kati ya makipa ambao uwezo wao unaonekana wa kawaida sana kudakia timu kubwa kama Liver na Barca.... Liverpool baada ya kumsajili kipa kutoka Sunderland Simon Mignolet inaonekana muda wa Reina kuwepo umeisha. Kwa mujibu wa taarifa kutoka mitandao mbalimbali nchini Uingereza, inasemekana Reina yuko mbioni kujiunga na timu ya Napoli kwa mkopo. Napoli inayofundishwa na kocha wa zamani wa Liverpool, Rafa Benitez inatarajiwa kukamilisha uhamisho huo ndani ya siku chache. Reina anatarajiwa kwenda Italia kwa ajili ya vipimo kabla ya kuhamia rasmi Napoli.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates