Home Unlabelled KALI YA SIMON COWELL
KALI YA SIMON COWELL
By burudanibuzz At July 31, 2013 0
Moja kati ya watu ambao wamefanya kazi kubwa kunyanyua muziki hasa wa pop & RnB ni Simon Cowell. Rumours mtaani ni kwamba milionea huyo sasa anategemea kupata mtoto lakini mwanamke mwenye ujauzito huo ni mke wa rafiki yake. Mwanamama mwenye ujauzito wa Simon anaitwa Lauren Silverman ambaye ni mke wa rafiki yake Cowell anayeitwa Andrew. Taarifa za kidaku kutoka familia ya Andrew na Lauren zinadai wawili hao wamekuwa katika mahusiano yasiyoridhisha kwa muda mrefu na kuna uwezekano suala la talaka kati yao lipo karibu. Simon Cowell anahusika katika vipaji vikubwa kama Westlife, One Direction, kupitia kampuni yake ya Syco huku staa kama Leona Lewis akiwa zao la shindano la UK X-Factor ambalo lilianzishwa na Cowell.