CHAJI SIMU KWA MKOJO




Unahisi mkojo hauna dili????? Kama una fikra hizo naomba uzifute kwa sababu wataalamu kutoka Bristol nchini Uingereza wamegundua njia ya kuchaji simu kwa kutumia mkojo. Sasa mkojo utapata kazi mbadala hasa kwa nchi yenye matatizo ya umeme kama Tanzania ambapo huenda teknolojia hii itafika suala la simu kuishiwa chaji litakuwa ndoto.
Ugunduzi huo umetokana na kazi iliyofanywa na wataalamu kutoa Bristol & West England Universities uliwawezesha wataalamu hao kuchaji simu waliyoweza kufanya nayo mawasiliano na kubrowse internet kwa muda.
Mmoja wa wataalamu Dr. Ioannis Ieropoulos amesema "It's an exciting discovery.
"Using the ultimate waste product as a source of power to produce electricity is about as eco as it gets."  Huku akielezea matarajio ya kuifanya huduma hiyo kuwa ya kudumu ambapo amependekeza kuwepo kwa vyoo (SMART TOILETS) ambavyo vitasaidia kuto huduma hiyo si kuchaji simu tu bali kutumika kama chanzo cha umeme kwenye mabafu pia.

Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates