

Mshiriki wa Tanzania kwenye jumba la big brother Africa (The Chase) Nando alitolewa mjengoni jana kutokana na kuvunja sheria za Big Brother. Mshiriki huyo juzi alianzisha ugomvi na Elikem na kwa mujibu wa Biggie jamaa ameshafanya makosa kibao ikiwemo kukutwa na silaha kama kisu na mkasi kwa nyakati tofauti. Mshiriki mwingine Annabel kutoka Kenya naye aliaga mashindano hayo kutokana na kura za kawaida zinazopigwa na watu kutoka nchi mbalimbali. Tanzania sasa imebakiwa na mshiriki mmoja Feza Kessy...Breaking News: Nando disqualified and Elikem gets a Strike. Get full story here: http://t.co/ZsBwGWXJ6x #BBATheChase pic.twitter.com/JjKx8UrhYu
— Big Brother Africa (@BigBroAfrica) July 28, 2013