Home Unlabelled MOYES KUTANGAZWA KOCHA MPYA MANCHESTER UNITED
MOYES KUTANGAZWA KOCHA MPYA MANCHESTER UNITED
By burudanibuzz At May 08, 2013 0
Masaa machache baada ya Sir Alex Ferguson kutangaza kwamba atastaafu mwishoni mwa msimu, kocha wa Everton David Moyes amepata ulaji wa kuhamia Old Trafford. Moyes mwenye miaka 50 amekuwa kocha wa Everton kuanzia mwaka 2002. Kocha huyo raia wa Scotland kama alivyo Ferguson ni mmoja kati ya makocha ambao wamekuwa wakitoa upinzani mkubwa kwenye ligi ya Uingereza huku timu kubwa zikijihadhari kila mara zinapocheza na Everton. Davi Moyes atahamia Man U mara baada ya msimu kwisha na kuna uwezekano kuondoka kwake kukachangia kwa kiasi kikubwa kuhama kwa nyota wa Everton kama Fellaini ambaye timu nyingi kubwa zinamhitaji. Ndani ya masaa 24 kocha huyo atakuwa amethibitishwa kuchukua nafasi hiyo kutokana na kocha mwingine aliyekuwa akipewa nafasi ya kumrithi Ferguson, Jose Mourinho kutopewa sapoti na viongozi wakuu wa United.