MOYES ASAINI MIAKA SITA

Kocha wa Everton, David Moyes amesaini mkataba wa miaka sita kuinoa Manchester United baada ya kocha Sir Alex Ferguson kutangaza kustaafu kufundisha soka. Pamoja na watu wengi kukosoa rekodi yake ya mechi za ugenini hasa akicheza na timu kubwa wachambuzi wengi na wadau wengine wa soka wameonyesha matumaini yao. Dwigh Yorke ambaye ni nyota wa zamani wa Manchester United amesema Moyes ndio chaguo sahihi kurithi mikoba ya Babu Fergie. Yorke amesema "When you look at all of the managers who are out there at this point in time, he fits the role perfectly".


LAUDRUP

 Naye David Moyes hakuwa na mengi ya kusema zaidi ya kutoa shukrani kwa Ferguson. Ikumbukwe  kuwa Moyes amepata nafasi ya kuifundisha Manchester kutokana na mapendekezo ya kocha anayeondoka Sir Alex Ferguson. Kwa upande wa Everton baada ya kukubali kuondoka kwa kocha wao huyo aliyekaa Everton kwa miaka 11 sasa wako katika mchakato wa kutafuta kocha mpya. Roberto Martinez anayeinoa Wigan Athletic anaonekana kama mtu sahihi wa kuchukua
MARTINEZ
nafasi itakayoachwa wazi na Moyes. Makocha wengine wanaotajwa ni pamoja na Michael Laudrup (Swansea), Mark Hughes na mchezaji wa timu hiyo Phil Neville.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates