CHELSEA, BENFICA KUKUTANA FAINALI EUROPA

SHUJAA LUIZ
MOHAMED SALAH
Timu ya Chelsea imejikatia tiketi ya kushiriki fainali za UEFA-EUROPA cup hapo jana baada ya kuifung FC Basle 3-1 Stamford Bridge. Ikicheza mbele ya mashabiki wa nyumbani Chelsea ilingara  kwa magoli ya Fernando Torres, Victor Moses na David Luiz kipindi cha pilidakika za 50, 52 na 59. Basle walianza kupata bao kupitia kwa Mohamed Salah dakika ya nyongeza (46) kabla ya mapumziko. Chelsea kwa mantiki hiyo itasafiri mpaka Amsterdam kucheza fainali dhidi ya Benfica ambayo ilipata ushidi kama wa Chelsea na kuiondoa Fenerbahce. 

Add caption
Mshambuliaji wa Benfica Oscar Cardozo alifunga magoli mawili kuihakikishia timu yake nafasi ya fainali licha ya kufungwa 1-0 kwenye mechi ya kwanza.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates