Baada ya kufungwa 3-1 kwenye uwanja wao pale Nou Camp, kesho Barcelona inatafuta njia ya kuondoa aibu hiyo itakapokutana na Madrid kwa mara nyingine. Mechi ya keso inatofautiana kidogo na iliyopita kwa kuwa mechi ijayo itakua ya Ligi kuu almaarufu La Liga. Real Madrid iko nafasi ya 3 nyuma ya vinara Barcelona huku nafasi ya pili ikishikiliwa na Athletico Madrid. Real inazidiwa pointi 16 na Barcelona na huenda imeshaanza kupoteza matumaini ya kuchukua ubingwa hata hivyo hawatataka kupata aibu kwenye uwanja wao wa nyumbani jambo linalofanya pambano hilo kuwa na msisimko wa aina yake. Barcelona inahitaji kulipa kisasi kwa kipigo walichopata huku Madrid nao wakihitaji kuthibitisha kuwa hawakubahatisha. Katika mechi 165 ambazo zimekutanisha Real Madrid na Barcelona (LA LIGA) kuanzia mwaka 1929,Madrid imeshinda mara 69, Barca mara 64 huku wakitoka sare mara 32.