EL-SHAARAWY AJIFUNGA AC MILAN


Stephan El-Shaarawy mchezaji wa AC Milan mwenye miaka 20 tu amesaini mkataba mpya wa kubaki na timu yake hiyo. Stephan mwenye asili ya Misri amekuwa moto wa kuotea mbali katika msimu huu huku akifunga magoli muhimu kwa timu yake na akichangia magoli mengine mengi akisaidiana vyema na Kevin Prince Boateng.Stephan amesaini mkataba mpya utakaomfanya abaki AC Milan hadi mwaka 2018. Ikumbukwe kuwa El-Shaarawy ndiye anayeongoza kwa ufungaji wa mabao AC Milan
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates