CHRIS ASUBIRIWA GHANA

Chris Brown kwa mara nyingine anakuja Afrika na safari hii ni zamu ya Ghana kumshuhudia LIVE. Mwanamuziki huyo ambae alikuwa kwenye tuzo za KORA Ivory Coast na baadae akaenda Nigeria anatarajiwa kufanya shoo kwenye sherehe za uhuru wa Ghana zitakazofanyika tarehe 6 March mwaka huu. Ghana ambayo ni nchi ya kwanza Afrika kupata uhuru kutoka kwa wakoloni ilijipatia uhuru wake tarehe 6 Machi, 1957 naChris anatrajiwa kuwasili siku moja kabla ya sherehe hizo yaani Machi 5.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates