Timu namba moja kwa ubora duniani Barcelona jana ilitia aibu nyumbani
baada ya kufungwa na Real Madrid mabao 3-1. Kwa mantiki hiyo Barcelona
imetolewa ktk michuano ya kombe la mfalme maarufu kama Copa Del Rey
kwa jumla ya mabao 4-2. Barcelona walikua na matarajio makubwa ya
kuingia fainali baada ya kutoka sare ya 1-1 kule Santiago Bernabue
lakini mambo yalienda kinyume na wakajikuta wanaangukia pua. Cristiano
Ronaldo alifunga magoli mawili katika pambano hilo huku beki Raphael
Varane akipachika bao la tatu. Goli la Barcelona lilifungwa na Jordi
Alba na matokea hayo yanakuja wiki moja baada ya Barca kuchapwa 2-0 na
AC Milan. Barcelona baada ya kuondoka kwa kocha mkuu Tito Vilanova
aliyeko Marekani kwenye matibabu timu hiyo imekua ikisuasua kwa muda
sasa.