WELBECK ASAINI ARSENAL, FALCAO AJIUNGA MAN U

Dirisha la usajili barani Ulaya limefungwa huku klabu ya Arsenal ikipata sahihi ya aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester United, Danny Welbeck. Welbeck mwenye miaka 23 anaelekea kwa washika mitutu wa London kujaribu kuondoa tatizo la kukosa mshambuliaji ambalo limekuwa likiisumbua klabu hiyo.
Mchezaji huyo alijiunga na Manchester United msimu wa 2005-2006 na baadaye kupelekwa kwa mkopo katika klabu za Preston North End na Sunderland kabla ya kuanza kupata nafasi kwenye kikosi cha mashetani wekundu 2011. 
 Wakati huo huo, klabu ya Real Madrid imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Mexico na Manchester United Javier Hernandez "Chicharito". Chico anajiunga na Madrid kujaribu kurejesha kiwango chake kilichomvutia Sir Alex Ferguson kumsainisha mshambuliaji huyo. Uhamisho wa Hernandez umekuja kama mshituko kwa mashabiki na wafuatiliaji wengi wa soka duniani kote kutokana na kikosi cha Madrid kusheheni mastaa na namba ya Hernandez inaonekana kuwepo mashakani kama ilivyokuwa Manchester.

Klabu ya Manchester United ambayo hadi sasa inachecehmea kwenye ligi kuu ya Uingereza imefanikiwa kumsajili kwa mkopo Radamel Falcao kutoka klabu ya AS Monaco ya Ufaransa. Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Colombia amesajiliwa na kocha wa Man United kujaribu kuisaidia klabu hiyo kurudisha heshima yake kutokana na matokeo mabovu siku za hivi karibuni.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates