ROONEY NAHODHA MPYA ENGLAND




Mshambuliaji na nahodha wa klabu ya Manchester United, Wayne Mark Rooney amechaguliwa kuwa nahodha wa tiu ya taifa ya Uingereza. Rooney mwenye miaka 28 anachukua nafasi iliyoachwa wazi na kiungo wa Liverpool Steven Gerrard aliyestaafu soka la kimataifa mara baada ya kumalizika fainali za kombe la dunia zilizofanyika nchini Brazil na kumalizika Julai 13 mwaka huu. 

Mchezaji huyo amekichezea kikosi cha Three Lions mechi 90 huku akifunga magoli 40. Rooney aliitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha wakubwa Uingereza akiwa na miaka 17, alicheza mechi yake ya kwanza Februari 12,2003 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Australia.


Rooney huenda akaanza majukumu yake ya unahodha kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Norway Septemba mwaka huu kabla ya kikosi cha Roy Hodgson kuanza kampeni ya kusaka tiketi ya kushiriki kombe la mataifa barani Ulaya (EURO)
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates