RVP KUWA NAHODHA MPYA MAN UNITED


Huku mashabiki wa Manchester United wakisubiri kutangazwa kwa kocha atakayehukua nafasi ya Davi Moyes aliyetimuliwa Old Trafford, habari kutoka Uholanzi zinadai kuwa Robin Van Persie huenda akavaa kitambaa cha unahodha iwapo Louis Van Gaal atapewa mikoba ya kuinoa klabu hiyo. Van Gaal ni kocha wa timu ya Uholanzi kwa sasa na alimteua Robin kuchukua unahodha wa timu ya taifa takriban miezi kumi iliyopita. Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali nchini Uholanzi, Van Gaal na Van Versie wana mahusiano mzuri na huenda Mdachi huyo akapewa Unahodha mara baada ya Van Gaal kutangazwa rasmi.

Endapo Van Persie atatajwa nahodha wa United, kuna uwezekano wa kutokea kwa msuguano baina ya mashabiki na wachezaji wa timu hiyo hasa hiyo hasa mashabiki wa Kiingereza ambao wanahitaji mshambuliaji Mwingereza Wayne Mark Rooney kupewa kitambaa hicho. Manchester United bado iko kwenye mazungumzo na Van Gaal ambaye atakuwa huru baada ya kuiongoza Uholanzi katika michuano ya kombe la dunia itakayoanza June 12 hadi Julai 13.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates