Home Unlabelled LIVER YAVUTWA SHATI
LIVER YAVUTWA SHATI
By Iam Owino At May 05, 2014 0
Matumaini ya Liverpool kuendelea kutimulia vumbi timu nyingine kuelekea ubingwa wa ligi kuu Uingereza yametiwa doa na timu ya Crystal Palace baada ya kulazimishwa sare ya 3-3 pale Selhurst Park. Dakika 18 zilitosha kuipa Liverpool goli la kwanza lililowekwa kimiani na Joe Allen, magoli mengine ya Liver yalifungwa kipindi cha pili na Daniel Sturridge pamoja na Luis Suarez dakika ya 53 na 55 ya mchezo. Delaney aliipa Palace bao la kwanza dakika ya 79 na baadaye Gayle kufunga mabao mawili dakika ya 81 na 88 na kupeleka kilio Anfield. Mchezaji bora wa ligi kuu ya Uingereza Luis Suarez alishindwa kujizuia na kukutwa akidondokwa na machozi kufuatia matokeo hayo. Liverpool hata hivyo inaongoza ligi ikiwa na pointi moja mble ya Manchester City inayoshika nafasi ya pili lakini City ina mchezo mmoja mkononi hivyo majaliwa ya Liver kuchukua ubingwa yanabaki kuombea Man City kupoteza mchezo hata mmoja huku wao wakishinda mchezo mmoja waliobaki nao.