Home Unlabelled GIGGS KOCHA-MCHEZAJI, VIDIC AAGA
GIGGS KOCHA-MCHEZAJI, VIDIC AAGA
By Iam Owino At May 06, 2014 0
Ligi kuu ya Uingereza inaelekea ukingoni huku Manchester United hapo jana usiku ikicheza mechi ya mwisho ambapo kati ya vitu vilivyovuta macho ya watu wengi ni kocha wa muda Ryan Giggs kuingia na kucheza huku Nemanja Vidic akiaga wachezaji na mashabiki wa United waliokuwepo uwanjani usiku wa jana.Giggs ambaye alichukua mikoba aya kocha aliyetimuliwa David Moyes aliingia uwanjani na kushangiliwa na mashabiki waliofurika Old Trafford kushuhudia mechi hiyo ya mwisho. Kocha Giggs alianzisha wachezaji makinda huku majina mengi makubwa yakiachwa nje katika pambano lililoshuhudia kinda James Wilson akipachika mabao mawili huku Robin Van Persie akiifungia United goli la tatu.