
Biashara hiyo inaweza kushuhudia Dre akiweka kibindoni kiasi cha dola Bilioni moja kutokana na dili hilo linalokadiriwa kufikia 3.2 $Billion. Dr Dre anashikilia nafasi ya pili kati ya wanahip hopmatajiri zaidi ulimwenguni akiwa na utajiri wa $ Milioni 55o na endapo dili lake na aplle litakamilika atakuwa msanii wa kwanza kufikia kiasi hicho cha utajiri. Tofauti na biashara, Dre ni prodyuza pamoja na msanii wa hip hop huku akiwa kwenye game kwa miaka takriban 30.
