![]() |
Letterman & Barack Obama |
![]() |
Bieber |
![]() |
Beyonce kweye show |
Watangazaji wa vipindi vya runinga na redio wamekuwa na ushawishi pamoja na mvuto mkubwa katika jamii mbalimbali na David Letterman ni mmoja kati ya wanahabari wanaotambulika sana ulimwenguni kwa kazi zake. Letterman mwenye miaka 66 kwa sasa amekuwa mwendesha kipindi cha televisheni "Late Show David with Letterman" iliyoanza kuoneshwa mwaka 1982 katika kituo cha CBS nchini Marekani. Baada ya kuendesha kipindi hicho kwa miaka mingi na mafanikio makubwa David anatarajia kuacha utangazaji wa kipindi hicho mkataba wake wa sasa utakapoisha August 2015. Letterman amekuwa maarufu duniani kote kutokana na kufanya mahojiano na watu maarufu duniani huku mara kwa mara akiingia katika migogoro na watu mashuhuri kama akina Oprah Winfrey na wengine wengi.
Taarifa za awali zinadai kuwa nafasi ya Letterman itachukuliwa na Craig Ferguson