Home Unlabelled CITY YAFA MBELE YA BARCA
CITY YAFA MBELE YA BARCA
By burudanibuzz At February 19, 2014 0
Mabao mawili ya Lionel Messi na Daniel alves yalitosha kuipa Barcelona ushindi muhimi wa 2-0 mbele ya Manchester City kwenye uwanja wa Etihad. Faulo aliyochezewa Messi na beki wa Man city, Martin Demechelis dakika ya 53 ya mchezo ilishuhudia beki huyo akioneshwa kadi nyekundu kabla ya Messi kupiga penalti iliyowaweka Barca mbele kwa bao 1. Alves alifunga goli la pili na kuwaach city na kazi ngumu ya kusafiri hadi Camp nou kujaribu kurekebisha makosa yao au waage michuano hiyo. Katika mechi nyingine, Paris St germain ilishinda 4-o mbele ya Bayern Leverkusen huku Zlatan Ibrahimovic akifunga magoli mawili.