MATA ANYEMELEWA NA UNITED

Wakiwa bado wanajiuliza makosa yaliyosababisha kupigwa 3-1 na Chelsea huku huo ukiwa ni mwendelezo wa matokeo mabovu ya Manchester United, kocha David Moyes anatafuta saini ya kiungo mshambuliaji wa Chelsea raia wa Hispania Juan Mata. Habari za chini ya kapeti zinadai kuwa Moyes ametuma ofa ya pauni milioni 37 kumpeleka Mata Old Trafford baada ya kukosa namba katika kikosi cha Jose Mourinho. Tangu kuwasili kwa Mourinho, Mata ambaye msimu uliopita alikua nguzo muhimu ya The Blues na kuibuka mchezaji bora wa msimu amepokonywa namba kutokana na Mourinho kupendelea kumtumia Oscar kama namba 10 nafasi ambayo anaicheza Mata.
Mata huenda akatimkia timu yoyoyte atakayopewa nafasi ya kucheza mara kwa mara lakini swali likibaki kwenye utayari wa Jose Mourinho kukubali staa huyo aondoke.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates