BIEBER HATARINI KUFUKUZWA MAREKANI

Msanii Justin Bieber yuko hatarini kurudishwa kwao Canada baada ya wananchi wa Marekani kuiomba serikali ya Rais Barack Obama kumuondoa nyota huyo nchini mwao kutokana na matatizo ya kila mara ambayo Justin anasababisha. Watu zaidi ya laki moja wamesaini maombi ya kumuondoa Justin idadi ambayo inamaanisha kazi inabaki kwa ikulu ya Marekani kupima uzito wa mambo yalivyo kabla ya kutoa maamuzi. Makosa ya hivi karibuni ya msanii huyo yanajumuisha kulewa, kuendesha gari bila kuwa na leseni halali, matumizi ya dawa za kulevya, pamoja na uendeshaji wa gari akiwa amelewa. Msemaji wa ikulu ya Marekani (White House) Matt Lehrich amesema hoja hiyo ambayo imepitia katika mtandao wa White house, itaangaliwa kwa umakini na wataalamu kabla ya kutoa maamuzi. Wamarekani wengi wanadai Justin ni mfano mbaya kwa vijana wengi ambao pia ni mashabiki wake. Staa huyo alishika nafasi ya pili miongoni mwa mastaa walio chini ya miaka 30 walioingiza fedha nyingi mwaka jana akiwa nyuma ya Lady Gaga.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates